Amezaliwa, mwokozi wetu
Ili tuuone mjia mpya
Imanueli, huyu Yesu Mwana
Alikwishwa tabiriwa kwetu.
Kengele zalia,
kwa utukufu
Mwana Kondoo wa Mungu amezaliwa
Kweli furaha kubwa wote ulimwengu
Mamajusi tuwaige tumshangilie Mwana.
Mbinguni furaha, malaika wasifu
Mwana wake ashuka, kuukoa ulimwengu
Na tumpokee, tumpe na zawadi
Ili aishi, zetu nyoyoni.
Kengele zalia,
kwa utukufu
Mwana Kondoo wa Mungu amezaliwa
Kweli furaha kubwa wote ulimwengu
Mamajusi tuwaige tumshangilie Mwana.
Bahati gani, pale Bethlehemu
Horini kafanya, makao yake
Asiye kosa, Mwana wa Mungu
Ili tuweze pata uzima milele.
Kengele zalia,
kwa utukufu
Mwana Kondoo wa Mungu amezaliwa
Kweli furaha kubwa wote ulimwengu
Mamajusi tuwaige tumshangilie Mwana.
NB: Meanwhile, I have a small ask:- I am running a campaign that will enable me launch my two books in February, end, 2024. I humbly ask of your donations of 20KES/20Kshs/20bob, towards this. The campaign is dubbed #20BobSanaa. Thanks in advance. You can also support by liking and sharing this content, or by buying these books using the following links:
‘A Funeral Dress for
Nyasuguta’ available at: https://nuriakenya.com/product/a-funeral-dress-for-nyasuguta-by-mark-mwangi/
‘Love Told, Poetry
Souled, Family Bold’ – available on Amazon Kindle at http://shorturl.at/hzALY
Buy Good Till Number: 9080911, Gatere Mwangi
Send Money: 0708 276 622, Mark Gatere
Comments
Post a Comment