Mungu wangu nimefika mwisho
Taabu mingi zimevunja kingo
Machozi sasa yamejazaa mto
Omba omba waniita mtu ovyo.
Nimelia
nimechoka
Yangu machozi yameisha
Sasa natazamia huruma yako
Nisizame Baba nyosha mkono.
Mungu wangu
niokoe
Zigo langu ulitwae
Chozi langu lipanguse
Neema yako – nishirikishe.
Tumaini langu kapunguka leo
Wasiwasi nao kanikaba koo
Tabasamu kawa mgeni uso
Furaha kanitaliki macheo.
Nimelia
nimechoka
Yangu machozi yameisha
Sasa natazamia huruma yako
Nisizame Baba nyosha mkono.
Mungu wangu
niokoe
Zigo langu ulitwae
Chozi langu lipanguse
Neema yako – nishirikishe.
Wanicheka walokuwa marafiki
Wamenitoroka sababu ya dhiki
Majirani kwao miye mgeni
Fakiri kawa wangu shemeji.
Nimelia
nimechoka
Yangu machozi yameisha
Sasa natazamia huruma yako
Nisizame Baba nyosha mkono.
Mungu wangu
niokoe
Zigo langu ulitwae
Chozi langu lipanguse
Neema yako – nishirikishe
Dhambi, deni zifutilie
Aibu yangu uiondoe
Moyo wangu nautulie
Daima yangu – unishibishe.
Nimelia
nimechoka
Yangu machozi yameisha
Sasa natazamia huruma yako
Nisizame Baba nyosha mkono.
Mungu wangu
niokoe
Zigo langu ulitwae
Chozi langu lipanguse
Neema yako – nishirikishe
Comments
Post a Comment